HOTUBA YA SHEREHE MIAKA 25 YA CHUO CHA MAFISA - TANZANIA TERRITORY {2000-2025}
COLONEL SAMUEL MKAMI Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu, Maafisa, Makadeti, na wafanyakazi, na ndugu zetu wote katika Kristo, Kwa furaha na shukrani kuu, tunasimama mbele ya Mungu leo hii kuadhimisha miaka 25 ya chuo chetu cha maafisa tangu chuo hiki kianzishwe mwaka 2000. Ni neema kubwa na si kwa uwezo wetu, bali ni kwa mkono wa Mungu aliyetuongoza hatua kwa hatua mpaka tumefika hapa. Kwanza, tunamshukuru Mungu Baba yetu kwa kuwa ndiye aliyepanda mbegu ya wito wa kuanzisha chuo hiki. Kupitia maono ya waanzilishi na uongozi wa Kanisa, ulikuwa kuwa ni lazima kanisa liwe na viongozi waliofundishwa vizuri ili kubeba maono ya mwokozi wetu na kufanya ukristo uwe na thamani kubwa mioyoni mwa watu wa Mungu. Na waanzi...